Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Afrika yahitaji mbinu za mnepo kukabili mabadiliko ya tabianchi
Mbinu za kujengea jamii mnepo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lazima ziimarishwe, wamesema washiriki wa mjadala wa ngazi ya juu kuhusuuhakika wa upatikanaji wa chakula Afrika ulioandaliwa na serikali ya Rwanda mjini Kigali kwa ushirikiano na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, kamisheni ya Muungano wa Afrika, Benki ya maendeleo Afrika, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD na Benki ya Dunia. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.
Mbinu za kujengea jamii mnepo zinahitajika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Afrika-FAO