Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

WFP/Photolibrary

Dkt Agnes Kijazi: Hali ya hewa haina mipaka, ni muhimu nchi zote tushirikiane.

Mkutano wa sayansi, teknolojia na ubunifu unakunja jamvi hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wabunifu wa sayansi na wabobevu wa teknolojia wamejadiliana kwa siku mbili.  Miongoni mwao ni Dkt Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania ambaye ni mmoja wa wajumbe 10 wa jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa la kutoa ushauri kuhusu jinsi sayansi na teknolojia inavyoweza kutumika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Sauti
2'29"