Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Kikao chamwisho cha mkutano wa COP24 Katowice, Poland,16 Disemba 2018.
UNFCCC/James Dowson

Baada ya vuta ni kuvute ya wiki mbili muafaka wafikiwa COP24

Baada ya wiki mbili za majadiliano ya makundi zaidi ya 200 yaliyokusanyika Katowice, Poland kwa ajili mkutano wa Umoja wa  Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi , COP24 ,yameidhinisha  muongozo wa utekelezaji wa mkataba wa Paris wa mwaka 2015, wenye lengo la kupunguza ongezeko ka joto duniani kuwa nchini ya nyuzi joto 2 ikilinganishwa na viwango vya kabla ya wakati wa viwanda.