Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mabadiliko ya Tabianchi
Akiwa COP24 Guterres ataja mambo manne muhimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 24 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP24 huko Katowice, Poland hii leo na kutaja mambo makuu manne anayoamini ni muhimu ili kubadili mwelekeo wa sasa wa tabianchi.
03 Disemba 2018
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo Siraj Kalyango anaangazia
-Kuanza kwa mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi COP 24, Umoja wa Mataifa ukihizima ufadhili na kasi ya kupambana na mabadiliko hayo
-Siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu , je ni yapi yanayomkabili mtu anayeishi na ulemavu? tutabisha hodi Kagera Tanzania
-Ngozi ya samaki aina ya sangara mali kubwa nchini Kenya kulikoni
-Makala tunaendelea na ibara za tamko la haki za binadamu leo ni ibara ya 23 ikiangazia haki za wafanyakazi wa ndani