Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Ukame na ukosefu wa chakula umesababisha warendile wasake misaada

Mabadiliko ya tabianchi duniani yamekuwa mwiba kwa kila jamii duniani zikiwemo zile za wafugaji ambazo huhamahama ili kusaka siyo tu malisho bali pia kusaka mahitaji yao ikiwemo maji na chakula.Mvua zimebadili mwelekeo, kiangazi ni kirefu kupita kiasi.  Ili kufahamu  kiwango cha athari hizo, Flora Nducha amezungumza na Bi Khoboso Argura Adichareh kutoka jamii ya warendile, katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya ambapo ameangazia kile kilichowakumba  na kwanza anaanza na madhara wanayoshuhudia.

Sauti
4'2"