Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya Tabianchi
Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linataka uhifadhi wa mazingira kwa kuchukua hatua muafaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio  Guterres akiwa ziarani katika nchi zilizoko ukanda wa pasifiki anapaza sauti ya kile kinachopaswa kufanywa kwa ubia ili kulinda sayari dunia kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J Mohammed akihutubia Baraza la Usalama wakati wa kikao cha kusongesha amani na usalama kilichojikita kwenye masuala ya kuelewa na kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi.
UN/Eskinder Debebe

Mabadiliko ya tabianchi ni kichocheo tosha cha mizozo-UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuangazia masuala ya tabianchia na athari zake kwa usalama ambapo Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo amesema, “ni lazima tuelewe mabadiliko ya tabianchi kama suala moja katika mkusanyiko wa vichocheo ambavyo vinaweza kusababisha mzozo” akiongeza kuwa huongeza mzigo juu ya hali dhaifu ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.