Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

TANZBATT 9

Lugha ya Kiswahili inatusaidia sana kwenye ulinzi wa amani DRC- Luteni Kanali Mley 

Lugha ya Kiswahili hivi sasa ni lugha ya kimataifa ikiwa imetengewa siku yake mahsusi ya kuadhimishwa ambayo ni tarehe 7 Julai kila mwaka. Wakati wa maadhimisho ya mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay alisema uamuzi wa Baraza Kuu la UNESCO kutambua lugha ya kiswahili kimataifa ulizingatia mambo kadhaa ya msingi ikiwemo nafasi ya lugha hiyo katika kusongesha amani.

Sauti
3'49"

22 JULAI 2022

Hii leo jaridani kubwa ni kutiwa saini huko Istanbul Uturuki kwa makubaliano baina ya Urusi, Ukraine na Umoja wa Mataifa ya kuwezesha nafaka na vyakula kutoka Ukraine viweze kusafirishwa kupitia Bahari Nyeusi. Shuhuda wa Umoja wa Mataifa kwenye utiaji huo saini si mwingine bali ni Katibu Mkuu mwenyewe wa UN, Antonio Guterres.

Sauti
12'59"