Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

14 JULAI 2022

Jarida la leo lina Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Jifunze Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi, Leah Mushi anamulika wito wa UNHCR wa kutaka sitisho la mapigano huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako watu wanauawa na maelfu wanafurushwa. Kisha anamulika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuwa ujira wa wanawake kwenye sekta ya afya ni wa chini kulinganisha na wanaume hata kama wako katika ngazi moja na mwisho ni wito kutoka UNCTAD wa kutaka bara la Afrika lisitegemee tu mazao na madini kupata fedha za kigeni bali iuze bidhaa za kihuduma.

Sauti
12'15"