Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UN

Kiswahili sasa kifundishwe vizuri shuleni

Tukigeukia sasa siku ya Lugha ya Kiswahili duniani itakayoadhimishwa Alhamisi ya wiki ijayo Julai 7 mmoja wa wakaazi wa Chukwani Zanzibar Ali Yusuf Mwarabu anasema hatua ya lugha hiyo kutambulika kimataifa kwanza ni Fahari kubwa kwa Wazanzibari lakini pia itakuwa ni fursa nzuri kwa wageni wanaoipenda kujifunza kwa urahisi kuanzia waliko na hata kufunga safari kwenda kisiwani humo.

 “Kwa wageni wengi wakija huwa wanapenda kusoma Kiswahili sasa kama kitakuwa kimeenea kila mahali itakuwa ni rahisi kwao pia wataanza kukisoma hukohuo kwao badala ya kutoka kwao kuja kukitafuta huku” 

Sauti
1'35"

01 Julai 2022

Hii leo jarida limejikita katika suala la Kiswahili kuwa lugha ya kimataifa na kuelekea kilele cha maadhimisho tarehe 7 Julai mwaka huu wa 2022. Utasikia mkazi wa Zanzibar akitoa maoni yake, halikadhalika mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na kisha mashinani mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Lakini kumbuka mkutano wa Bahari umefunga pazia hii leo huko Lisbon, Ureno na aliyemwakilisha Katibu Mkuu amesema kile kitakachofuatia, changamoto na fursa. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Sauti
9'58"