Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UNIC/Ahimidiwe Olotu

Tuzo za kimataifa za  lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert kutolewa kesho Tanzania

Nchini Tanzania kesho Jumatano kunatolewa tuzo na nishani za kimataifa za lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert. Tukio hilo litafanyika kwenye mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Dodoma, ambapo tukio linaleta pamoja washiriki na manguli na wabobezi wa lugha ya Kiswahili kutoka maeneo mbalimbali duniani, na litahusisha pia viongozi waandamizi wa serikali na mashirika ya kitaifa na kimataifa. Lakini tuzo hizo zilianzia wapi? Na ni nini mantiki yake?

Sauti
6'

19 Januari 2021

Leo Jumanne tunamulika utoaji wa chanjo ya COVID-19 kwa wakimbizi huko Jordan, kisha tunakwenda Cameroon kumulika wakimbizi waliofurushwa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kutokana na machafuko nchini mwao. Huko Brazil tunamulika jinsi miti inatumika kufuta machozi ya familia zilizopoteza jamaa zao kutokana na COVID-19.

Sauti
12'29"