Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UN News Kiswahili

Neno la Wiki-Ujana ni moshi

Sasa  ni Neno la wiki ambapo leo tutajifunza maana ya methali "Ujana ni Moshi" na mchambuzi wetu Josephat Gitonga, mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika kituo cha tafsiri na ukalimani 

Sauti
57"

24 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo kote duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awatakia kila la heri Waislam wote na kusema kwamba COVID-19 itaifanya Ramadhan ya mwaka huu kuwa tofauti kabisa

-Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema anatiwa hofu na kamatakamata na kubanwa kwa vyombo vya habari wakati huu wa janga la COVID-19 ambapo taarifa sahihi ni muhimu sana

Sauti
10'46"