Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UN News Kiswahili

Kiswahili chazidi kupasua mawimbi ya bahari na mawingu hata ughaibuni

Kiswahili! Kiswahili! Kiswahili! Kinazidi kupasua mawimbi ya bahari na mawingu na kuwa kivutio siyo tu kwa watu wazima bali pia watoto wadogo tena ughaibuni.

Huyu ni Braydon Bent, mchambuzi wa soka pengine mdogo zaidi barani Ulaya akijinasibu kwa lugha ya Kiswahili na kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wake. Mwenzangu Arnold Kayanda amezungumza na mwalimu wa Kiswahil wa Braydon aitwae John Jackson hivi sasa mkazi wa Ujerumani akianza kwanza kwa kuelezea kilichomvutia na Kiswahili.

Sauti
5'43"