Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

Saudi Arabia yakandamiza haki za binadamu

Saudi Arabia inaendelea kutumia sera na sheria zake kuhusu masuala ya usalama na  ugaidi kukandamiza wanaoipinga serikali.

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa leo na jopo la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi

Wataalamu hao wamesema viongozi wa dini, wanaharakati, wapinzani, waandishi wa habari na yeyote anayeipinga serikali nchini Saudi Arabia amejikuta akishikiliwa na vyombo vya dola na kuhukumiwa ambapo tangu mwezi Septemba mwaka 2017 zaidi ya watu 60 wamekamatwa.

UN yafuatilia maandamano Iran

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Iran ambako maandamano yanayodaiwa kuwa ni ya kupinga serikali yameingia siku ya tano huku watu 22 wakiripotiwa kuuawa.

Naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliulizwa iwapo Katibu Mkuu Antonio Guterres ana kauli yoyote kuhusu kinachoendelea Iran.

(Sauti ya Farhan Haq)