Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

Guterres kuzungumza na Rais Magufuli wa Tanzania

Kufuatia mauaji ya walinda amani 14 wa Tanzania huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC siku ya Alhamisi na wengine zaidi ya 44 kujeruhiwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres muda wowote sasa atazungumza kwa njia ya simu na Rais John Magufuli wa Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam.

(Sauti ya Balozi Augustine Mahiga)

Wapatieni makazi ya kudumu wahamiaji 1,300 Libya- UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limetoa  wito kwa serikali  zote duniani kutoa hifadhi wa kudumu kwa wahamiaji 1300 walioko katika mzingira magumu nchini  Libya.

Volker Turk  ambaye Kamisha msaidizi wa UNHCR kwa ajili ya ulinzi kwa wakimbizi amesema hali ya wahamiaji hao  nchini Libya ni ya kusikitisha sana, hivyo wahisani  wanahitajika kusaidia kuwapatia makazi ya kudumu.