Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

Msanii mzaliwa wa Zanzibar ashinda tuzo ya Sanaa ya Turner:IOM

Msanii wa Uingereza Lubaina Himidi ametambulika kimataifa juma hili baada ya kazi yake ya saana inayotanabaisha siasa za kibaguzi na mchango wake katika masuala ya kumbukumbu ya utumwa  na uhamiaji kushinda tuzo ya mwaka huu ya Turner ambayo ni tuzo ya kimataifa ya sana aza kuchora.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Bi Lubaina Himidi mzaliwa wa Zanzibar nchini Tanzania , kazi yake ya sanaa imetambulika kimataifa kufuatia habari za karibuni za wahamiaji kutoka barani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara kuuzwa mnadani Libya kama watumwa.

Kenya na Burundi miongoni mwa nchi 37 zinazohitaji msaada wa chakula- FAO

Mavuno mengi ya nafaka ulimwenguni bado hayajaweza kusaidia kuondokana na ukosefu wa chakula katika nchi 37 duniani, 29 kati ya hizo zikiwepo barani Afrika.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO iliyotolewa leo huko Roma, Italia ikiangazia matarajio ya mazao na hali ya chakula.

Ripoti imesema kuwa mavuno ya nafaka yako juu lakini ukame, mafuriko na mizozo isiyoisha vimesababisha nchi kama vile Somalia, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Kenya kuhitaji msaada wa chakula kutoka nje.

Dkt. Salim azungumzia hatma ya Mashariki ya Kati

Kufuatia mjadala unaoendelea kuhusu hatma ya mji wa Yerusalem huko Mashariki ya Kati na mustakhbali wa suluhu ya mataifa mawili ya Palestin na Israel kwenye ukanda huo, mwanadiplomasia nguli nchini Tanzania Dkt. Salim Ahmed Salim ametaja kile kinachopaswa kuzingatiwa ili amani iwepo.

Dkt. Salim ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, UNIC baada ya mazungumzo yake na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za msingi kwa watu wa Palestina, Dkt. Salim jijini Dar es salaam.