Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

Wanawake wawili katika mpangilio wa studio, wakiwa wameketi kwenye meza ya duara wakiwa na maikrofoni, wakishiriki katika majadiliano mbele ya mandhari yenye nembo UN .
UN News/Feissal Kirwa

Wavamizi wote waondoke DRC ili sisi ‘wakongomani’ tuendeleze nchi yetu – Bi. Kibuya

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasiaya Congo, DRC, shirika la kiraia la Congo Notre Avenir, yaani kwa kiswahili, Congo Mustakabali wetu linapigania haki ya amani kwa wanawake ili hatimaye waweze kushiriki katika kuendeleza familia zao kwa kushirikiana na familia zao, wakati huu ambapo mapigano mashariki mwa nchi yamesababisha ukatili ikiwemo ubakaji, na hata wanaume kuacha familia zao na kwenda msituni kupigana.