Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

13 MEI 2026

Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa António Guterres hii leo huko Addis Ababa nchini Ethiopia, wanawake wanaowasili Ulaya kufuatia ukeketaji wa lazima katika nchi zao, na mafunzo ya kutatua migogoro kwa njia mbadala Zanzibar.

Sauti
9'59"
UN News

AfroKids International ni tumaini kwa wanawake wakimbizi barani Ulaya - Farina

Wanawake wengi wahamiaji na wakimbizi kutoka Afrika wanaowasili barani Ulaya wakisaka usalama na maisha bora hujikuta wakikabiliwa na majeraha ya kiwewe, changamoto za lugha na kutengwa kijamii. Nchini Ujerumani, shirika lililoanzishwa na wakimbizi, la AfroKids International, linafanya kazi ya kuwapa matumaini na msaada wanawake hao, hususan manusura wa ukeketaji au FGM.

Sauti
3'19"