Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

UN News

Ni jukumu la wanawake na wanaume kuendeleza haki za kila mtu - Dkt. Rukia Nzibo

Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao. Feissal Kirwa wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyo.

Audio Duration
2'29"