Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

19 MACHI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo baada ya takribani wiki mbili mkutano wa 70 wa CSW70 unakunja jamvi.  Maudhui yalikuwa kuendeleza Haki, Sheria na Kuchagiza Hatua kwa ajili ya wanawake na wasichana, na sasa washiriki wanaeleza Idhaa hii wanachoondoka nacho.

Sauti
10'57"
Mwanamke katika mavazi ya kitamaduni ya Maasai amesimama mbele ya bendera kubwa ya UN Women kwa CSW70, ambayo inasema 'Haki. Haki. Hatua. Kwa Wanawake na Wasichana Wote'.
Mshiriki wa Mkutano wa CSW70 akiwa amesimama mbele bango lenye maudhui ya mkutano huo.

CSW70 ikifunga pazia washiriki waeleza wanachoondoka nacho

  • Tutoke kwenye vikao sasa tuingie kwenye utekelezaji
  • IPU na mikakati ya kufanikisha mabadiliko ya Katiba, sheria na tamaduni
  • Ushirikishaji wanaume ni jawabu mujarabu
  • Kujumuika na majaji na mahakimu wanawake kumetupatia matumaini.
  • Vijana wasiachwe nyuma kokote pale