Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

Wanawake wawili Waafrika wameketi kwenye meza ya mviringo yenye rangi ya bluu wakiwa na maikrofoni katika studio ya kurekodi, wakiwa na nembo ya Umoja wa Mataifa kwenye skrini ya bluu nyuma yao.
UN News

“Sauti ya Mama Mukongomani” inamuwezesha na kumlinda mwanamke wa DRC: Nelly Mbangu

Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ametoa ushuhuda wa jinsi wanawake wa Congo wanavyopambana kupaza sauti zao duniani. Alihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hal ya Wanawake Duniani (CSW70) ameelezea kazi ya shirika lake lisilo la kiserikali, liitwalo “Sauti ya Mama Mukongomani,” kililoundwa mwaka 2008.

17 MACHI 2026

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha CSW70. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka DRC.

Nelly ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.

Sauti
9'59"
UN News

“Sauti ya Mama Mukongomani” inamuwezesha na kumlinda mwanamke wa DR Congo: Nelly Mbangu

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW70, Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasa ya Congo DRC, ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.

Sauti
5'58"