Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

UN News

Vijana wachagiza hatua za haraka kuhusu haki za wanawake katika mkutano wa CSW70

Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana. Flora Nducha amekutana na baadhi yao kusikia maoni yao

Sauti
3'26"
Wanawake weusi wawili wameketi kwenye meza ya mviringo yenye maikrofoni katika studio ya utangazaji, wakiwa na skrini kubwa inayoonyesha nembo ya Umoja wa Mataifa nyuma yao.
UN News

Vijana wachagiza hatua za haraka kuhusu haki za wanawake katika CSW70

Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana.

Sauti
3'26"