Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW70

Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani
Mkutano wa 70 - CSW70

Kuanzia tarehe 9 hadi 19 Machi 2026, macho na masikio yataelekezwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambako kutafanyika Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70.

Hili ni jukwaa kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalojikita katika usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kinachotokea katika CSW huwa na mchango kwenye sheria, sera, ufadhili na uwajibikaji katika nchi mbalimbali na kwa vizazi tofauti.

Kinachomulikwa mwaka huu ni:  Haki, Sheria na Hatua kwa Wanawake na Wasichana wote, ikienda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani Machi 8.

09 MACHI 2026

Hii leo jarida la Umoja wa Mataifa linakuletea taarifa ya ufunguzi wa Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 jijini New York Marekani, mwaka huu kikibeba maudhui “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote”. Zaidi ya washiriki 9000 wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa na mashirika yake na wadau wengine wanatarajiwa kushiriki jukwaa hili litakalokunja jamvi 19 Machi likijumuisha mikutano ya kando 750.

Sauti
11'51"
Michelle Williams, mwimbaji mshindi wa tuzo ya Grammy na mwigizaji wa Broadway, anazungumza katika Ukumbi wa Baraza Mkuu la Umoja wa Mataifa wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ya 2026.
UN Wanawake/Ryan Brown

CSW70 yang’oa nanga ikisisitiza haki, haki ya kisheria na hatua kwa wanawake na wasichana

Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kimefungu pazia hii leo jijini New York Marekani, mwaka huu kikibeba maudhui “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote”. Zaidi ya washiriki 9000 wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa na mashirika yake na wadau wengine wanatarajiwa kushiriki jukwaa hili litakalokunja jamvi 19 Machi likijumuisha mikutano ya kando 750.

Sauti
4'