Vijana wanahitaji ajira, stadi na matumaini bila hivyo, ni rahisi kutumbukia kwenye uhalifu - Monica Juma
Pakua
Wakati dunia ikikabiliwa na ongezeko la uhalifu wa kupangwa, biashara haramu ya binadamu na matumizi ya dawa za kulevya, mwanamke kutoka Afrika Mashariki amepewa jukumu kubwa la kusaidia kuongoza mapambano ya kimataifa dhidi ya changamoto hizo.
Monica Juma, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), anavunja rekodi kwa kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika Mashariki na Kusini mwa dunia kushika nafasi hiyo ya juu katika taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
Pata mahojiano maalum na ya kina baina ya Flora Nducha wa Idhaa hii na Mkuu huyu mpya wa ofisi ya UNODC.
Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
9'13"