16 MACHI 2026
Pakua
Hii leo jaridani tunaangazia vita nchini Iran, sauti za vijana katika wiki ya pili ya mkutano wa CSW70, na mafunzo ya vitendo kwa vijana nchini Uganda kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki.
- Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike.
- Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'59"