25 SEPTEMBA 2025
Pakua
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.
- Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.
- Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awali tulijitahidi kujiuliza ‘Nini ni sahihi’ chini ya sheria ya kimataifa, leo tunashuhudia kwa wazi kuibuka kwa matumizi ya NGUVU ya kitaifa katika kusuluhisha migogoro. Hii ni njia ya giza na ya hatari sana inayotishia utawala wa sheria wa kimataifa tuliokubaliana kwa pamoja kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.”
- Kando ya hotuba za viongozi, kunafanyika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa Programu ya Dunia kwa ajili ya vijana. Je vijana kutoka Malawi wana ujumbe gani? Mwakilishi wao kwenye mkutano huu Rachel Mganga Wanangwa anasema, “Ujumbe kutoka vijana wa Malawi ni wekezeni kwetu, tusaidieni, shirikianeni nasi, na wanashiriki kwenye meza za mazungumzo ili kuhakikisha kuwa sauti zao zinawakilishiwa.”.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
11'20"