Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 SEPTEMBA 2025

02 SEPTEMBA 2025

Pakua

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa FAO Mjini Morogoro, uliokutanisha viongozi wa Serikali kutoka katika Taasisi zinazojihusisha na udhibiti na usalama wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.

  1. zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi wanachama zinapaswa kushughulikia tatizo hilo kwa “Kuwekeza katika afya ya akili, kwani kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”
  2. Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi na pole kwa wananchi wa sudan kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa ambayo imesababisha maafa katika kijiji cha Tarsin huko Jebel Marra nchini Sudan mwishoni mwa wiki.
  3. Nchini Afghanistan ambako idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea juzi jumapili, wafanyakazi wa misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanafikisha misaada kwa waathirika. Akizungumza na waandishi wa habari kutokea Kabul Afghanistan Indrika Ratwatte ambaye ni mwakilishi wa UN nchini humo amesema “Sio rahisi kufika maeneo yaliyoathirika kitu ambacho kinawafanya majeruhi waendelee kufungiwa.” Ametaja juhudi za haraka zinazofanyika ni pamoja na kuzika miili ya waathirika na kufukia mifugo ili kuzuia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka.”.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'53"