Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 AGOSTI 2025

15 AGOSTI 2025

Pakua

Jaridani leo tunaangazia mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, na vidokezo vya malezi salama ya watoto. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?

  1. Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, Uswisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.
  2. Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni  mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.
  3. Makala ninakukutanisha na Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania ambaye baada ya mafunzo ya siku tatu ya uchumi rejeleshi katika mkoa wa Mtwara, Kusini-Mashariki mwa Tanzania alizungumza na Godlove Makunge Muasisi na Mkurugenzi wa kampuni ya kuzoa taka na usafi wa mazingira, iitwayo Shikamana Investment. Bwana Makunge anaanza kwa kuelezea mtazamo wa jamii kwake baada ya kuamua kuanza kuzoa taka.
  4. Na katika Radwa Ahmed, Mkimbizi kutoka Sudan ambaye alianza kwa kuoka mikate kwa ajili ya familia yake, na kwa ufadhili wa shirika la Umoja wakimbizi Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameweza kuigeuza talanta yake kuwa biashara ya kuuza mikate na kuajiri wakimbizi wenzake.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
9'43"