Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR Tanzania inaendesha zoezi la tathmini ya wakimbizi kutoka Burundi

UNHCR Tanzania inaendesha zoezi la tathmini ya wakimbizi kutoka Burundi

Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii.

Juhudi kama hizo zinaendelea hivi sasa huko katika kambi ya wakimbizi ya Katumba iliyoko wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma, magharibi mwa Tanzania ambako kunafanyika tathmini ya kina kuhusu ulinzi na kutafuta suluhu ya pamoja kwa wakimbizi wa Burundi.

Akiwa amesimama katika mnara huko Katumba Afisa mawasiliano wa UNHCR Maimuna Mtengela anaeleza kuhusu zoezi hilo na ana ujumbe muhimu kwa wakimbizi wa Burundi. 

Pakua

Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii.

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
1'43"
Photo Credit
UN News