Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 AGOSTI 2025

08 AGOSTI 2025

Pakua

Jaridani leo tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza, na mradi wa mlo shuleni unaowezesha watoto kuendelea na masomo nchini Uganda. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?

  1. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu.
  2. Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali  umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi.
  3. Makala inakupeleka Mtwara, kusini mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.
  4. Na katika mashinani Patriciah Akinyi, Mwathirika wa jeraha linaloweza kuzuilika wakati wa kujifungua ambaye pia ni mnufaika wa matibabu ya upasuaji wa kurekebisha jeraha hilo la fistula nchini Kenya inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA, anasimulia kilichomkumba.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'56"