05 AGOSTI 2025
Pakua
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.
- Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.”
- Tukirejea Geneva, Uswisi unakofanyika mkutano utakaweka mwelekeo wa jinsi ya kukabiliana na uchafuzi unaotokana na plastiki duniani, Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Duniani, UNEP, ameonya kwamba, “uchafuzi wa plastiki tayari upo katika mazingira, baharini, na hata katika miili yetu. Tukizidi kuendelea kwa mwelekeo huu, dunia yote itazama katika uchafuzi wa plastiki.”
- Na mashinani leo tuko katika shoroba za makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wageni hutoka kila pembe ya Dunia kutembelea jengo hili la kihistoria. Mwalimu Maria Rulands ni mmoja wao.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'51"