Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

31 JULAI 2025

31 JULAI 2025

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.

  1. Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.
  2. Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mikono yake na kuweka kwenye fulana yake dengu zilizokuwa zimeanguka kutoka kwenye moja ya malori yanayoingiza chakula Gaza, hii ndio hali halisi.
  3. Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililotekelezwa hii leo na majeshi ya Urusi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo mtoto mwenye umri  wa miaka sita huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa..
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
9'56"