Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malezi ni kama kukunja shuka lakuvisha kwenye godoro, hakuna ajuae jinsi ya kulikunja

Malezi ni kama kukunja shuka lakuvisha kwenye godoro, hakuna ajuae jinsi ya kulikunja

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. 

Kama vile ambavyo hakuna njia au namna moja ya kipekee ya kumlea mtoto, basi pia hakuna njia moja ya kuwa mzazi. Kuwa mzazi ni safari ya kuelekea kusikojulikana bila kujali unatoka wapi.

Nikutokana na ukweli huo ndio maana shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF wakishirikiana na wakfu wa LEGO wanatekeleza mradi wa malezi ya wazazi ambapo wanazungumza na wazazi kutoka kila kona ya dunia ili kuonesha ni kwakiwango gani wazazi wanapitia changamoto na kwamba hakuna awaye yeyote mwenye majibu ya maswali yote.

Leah Mushi analetea simulizi ya mama kutoka nchini Afrika Kusini ambaye alipatwa na msongo wa mawazo baada ya kujifungua.

Annelisa Zimasa Swana ni mama wa watoto wawili kutoka Afrika Kusini akisimulia alivyogundua ni mjamzito alikuwa hajajiandaa kuwa mama. Anasema “Sidhani kama kunakitu kinaweza kukuandaa kuwa mama, nilikuwa naona kama ulimwengu wote unaniangalia mimi vile nitaenda kumlea mtoto. Nilisoma vitabu vingi, nilifanya mambo mengi kujiandaa, niliuliza maswali, lakini ulipofika muda wa kuingia uwanjani na kuanza malezi, ilikuwa stori nyingine kabisa.”

Mambo hayakuwa kama alivyotarajia kwani anasema "Nilivyojifungua mtoto wangu Yongama nilipata unyongofu baada ya kujifungua au Msongo wa mawazo,sikuwa na uhakika na kitu chochote, muda mwingi nilikuwa nakaa tu na kusema , hapana siwezi, sidhani kama nafaa kuwa mama.”

Maisha yaliendelea na akapata mimba ya mtoto wa pili,Anasema “Wakati najifungua mtoto wangu Etandwa, nilikuwa nimepata mimba kabla yake lakini iliharibika, na miezi mitatu tu kabla sijapata mimba nyingine mama yangu alifariki. Nilikuwa naogopa sana, lakini nilivyomshika mwanangu kwa mara ya kwanza, nikajipa moyo, nikasema, hali itaenda kuwa bora.”

Annelisa alitafuta msaada wa kitaalamu, “Sikuwa na uhakika na mambo mengi, lakini nikaja kutambua ya kwamba ili niwe mama bora ninahitaji kujijali mwenyewe, nilikuwa na dhamira ya dhati ya kutafuta msaada hasa kwa mimba yangu ya pili kutokana na hali niliyopitia katika mimba yangu ya kwanza. Nilikuwa na nia ya kwenda kupata tiba kwa mtaalamu wa kisaikolojia, nilitaka kuwa na mtu ambaye ninaweza kuzungumza naye juu ya kila kitu”

Baada ya kupata msaada wa kisaikolojia sasa Annelisa anafuraha.. na anasema anataka kuwa mama bora kwa watoto wake, anataka kuwafundisha kila kitu

Annelisa- Sabrina anasema “Ninachokipenda zaidi kama mama, ni kuona maendeleo ya ukuaji wao, ni nyakati ambazo na jivunia kuwa mama yao. Malezi ni kama kukunja shuka lakuvisha kwenye godoro , hakuna ajuae jinsi ya kulikunja.

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini. 

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
3'4"
Photo Credit
© UNICEF