23 JULAI 2025
Pakua
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Nigeria, na mradi wa nishati ya sola ya kusaidia wakulima nchini Ethiopia. Makala inakupeleka nchini Afrika Kusini na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Nigeria limesema litalazimika kusitisha msaada wake wa dharura wa chakula na lishe kwa watu milioni 1.3 kaskazini-mashariki mwa nchini hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu kutokana na ukata.
- Mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), ubalozi wa China wa kutumia nishati jadidifu ya jua kwa umwagiliaji, umeleta matumaini mapya kwa jamii za wakulima katika mkoa wa Sidama, kusini mwa Ethiopia.
- Katika makalaShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wakfu wa LEGO wametengeneza video yenye kuonesha familia nne na jinsi zinavyopambana na malezi ya Watoto wakiwa ni wazazi kwa mara ya kwanza. Leah Mushi ametazama video hiyo ya takriban dakika 30 na hapa anakuleta simulizi ya familia kutoka nchini Afrika Kusini.
- Na katika mashinani Noella Bagula, Mwanachama wa Alleluyah Safe Space ambaye ni mama mkimbizi wa ndani kutoka Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambako wanawake na wasichana wanapitia ukatili wa kijinsia katika migogoro. Bi Bagula anasema yeye sasa anajua jinsi ya kujilinda katika hali hatari kufuatia mafunzo yanayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya uzazi, (UNFPA) katika maeneo salama yaliyotengwa kwa ajili yao.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'58"