15 JULAI 2025
Pakua
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika juhudi za kinamama wajawazito na wanao kuambatana wakihudhuria kliniki kwa ajili ya mimbasalama. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.
- Takribani wapalestina 900 wameuawa katika wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa kimabavu na Israeli. wakihaha kupokea chakula. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Thameen Al-Kheetan amewaeleza waandishi wa habari Geneva, Uswisi kuwa watu 674 kati yao waliuawa wakiwa kwenye maeneo ya Mfuko wa Kiutu wa Gaza, (GHF) unaoendeshwa na Israeli na Marekani.
- Wakati huo huo Bwana Al-Kheetan amezungumzia mauaji yanayoendelea Ukingo wa Magharibi ikiwemo Yerusalemu Mashariki akisema, “muathirika mdogo zaidi ni Laila Khatib mwenye umri wa miaka miwili. Alipigwa risasi ya kichwa na jeshi la Israeli akiwa nyumbani kwao kijijini Ash-Shuhada.”
- Na leo ikiwa siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana Sangheon Lee, Mkurugenzi wa Ajira na Sera katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Ajira amesema …lazima tuhakikishe kuwa vijana wanapata ujuzi ambao ni wa maana, unaoweza kutumika katika mazingira mbalimbali, na unaotambuliwa na waajiri.
- Na kaika mashinani tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya, ambako kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Radio Domus, tunamsikia Dennis Mabuku, Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora katika kampuni ya BOC Kenya. Dennis anaeleza jinsi wanavyoichakata hewa ya kawaida na kuisafisha ili kupata hewa safi ya oksijeni kwa ajili ya matumizi ya hospitali na mabaki mengine kwa ajili ya matumizi mengine ya viwandani.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'57"