Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 JULAI 2025

11 JULAI 2025

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya nchini Burundi, na elimu ya upatanishi kwa jamii Ituri nchini DRC. Makala tunakupeleka nchini Kenya kumulika kilimo kichopatia riziki jamii na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki za wasichana.

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo Julai 11 limetangaza kwamba limeidhinisha Burundi kuwa imefanikiwa kuoandoa ugonjwa wa macho unaofahamika kama trakoma au vikope kama tatizo la kiafya la umma, na kuifanya kuwa nchi ya nane katika Kanda ya Afrika ya WHO kufikia mafanikio haya muhimu.
  2. Huko Djugu, jimboni Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wanawake wapatanishi waliopatiwa mafunzo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wamewezesha kurejea kwa mazungumzo baina ya jamii za Ezekere na Mandro ambazo kwa miaka kadhaa zilikuwa zinazozana.
  3. Katika makala Sharon Jebichii anatupeleka  Kaunti ya Tana River huko Kenya kumulika juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Kusimamia Ukame (NDMA) na Serikali za Kaunti katika kilimo, ambayo imeleta mabadiliko na matumaini kwa jamii za wakulima.
  4. Na kaika mashinani leo ikiwa siku ya idadi ya watu duniani, nampisha Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na AFya ya Uzazi, Dkt. Natalia Kanem akizungumzia umuhimu wa takwimu katika kuboresha maisha ya wakazi wa dunia!

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'59"