Pamoja na ulinzi wa raia, walinda amani wa UN Ituri waendesha kampeni ya afya..
Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wameendesha kampeni ya afya na kusaidia wakimbizi wa ndani kupata matibabu katika eneo hilo lililogubikwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi.
Tuko eneo la Rhoo hapa Ituri, kituo cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO hapa DRC.
Wamefunga hema kutoa huduma kwa wakimbizi wa ndani waliosaka hifadhi kukimbia machafuko makwao. Vipimo vikiendelea na wengine wakipatiwa dawa, Josee Ndroy Dz’Da, mnufaika hakuficha furaha yake.
(Sauti ya Josee Ndroy Dz’Da)
Daniel Lokana ni Rais wa Vijana hapa kambini Rhoo.
(Sauti ya Daniel Lokana)
MONUSCO pia husaidia kusafirisha hadi mji mkuu Bunia, wakimbizi waliopata majeraha makubwa.
Meja Zadid Bossais, Mkuu wa kitengo cha Afya cha Kikosi cha Bangladesh hapa Rhoo anasema kwamba jukumu letu ni ulinzi wa raia chini ya Umoja wa Mataifa. Lakini raia wanakabiliwa na shida nyingi za kiafya kwani eneo hili halina vituo vya afya vya kutosha kuhudumia watu wengi. Kwa ushirikiano na mamlaka za afya hapa tumeendesha kampeni mbili za afya kila siku kwa wakimbizi wa ndani. Tangu Januari hadi mei 2025 tumetoa huduma kwa wakimbizi wa ndani 400.
Pakua
Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wameendesha kampeni ya afya na kusaidia wakimbizi wa ndani kupata matibabu katika eneo hilo lililogubikwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
Audio Duration
1'48"