11 JUNI 2025
Pakua
Hii leo jaridani tunaangazia ajali mbayá ya meli katika pwani ya Djibouti lililokuwa linabeba wahamiaji wengi. Pia tunasalia hapa makao makuu ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18. Mashinani tutakwenda nchini DRC.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo.
- Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa Marekani.
- Makala tutasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na tutamsikiliza mmoja wa washiriki wa mkutano huu Bongani Simphiwe Makama kutoka Ufalme wa Eswatini ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na idhaa ya Kiswahili.
- Na katika mashinani fursa ni yake fursa ni yake Byamungu Rukera, Mwakilishi wa watu waliokimbia makazi yao huko Sake, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC akipazia sauti wakimbizi wenzake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA ambao wanawagawia chakula licha ya uhaba wa msaada huo.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'59"