Licha ya ukata UNICEF yajitahidi watoto nchini DRC warejee shuleni
Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi. Je ni kwa vipi? Anold Kayanda anasimulia zaidi.
UNICEF inasema hali ya kielimu si shwari kwa watoto katika majimbo ya Ituri, Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Tanganyika na kwamba licha ya ukata inaokumbana nao, kuanzia mwezi Januari mwaka huu kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha watoto kurejea shuleni.
Miongoni mwao ni Ketya Dunia Asingue mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa jimboni Kivu Kaskazini. Akiwa kwenye shule yao ya msingi ya Ngerero anasimulia hali ilivyokuwa.
Tayari UNICEF imezindua ombi la ufadhili wa dola milioni 57 ili kukabiliana na mgogoro wa mashariki mwa DRC. Hadi sasa, ni dola milioni 35.6 zimepatikana, na kuna pengo la ufadhili la dola milioni 22.