Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 FEBRUARI 2025

11 FEBRUARI 2025

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda kumulika ni kwa nini Uganda imekivalia njuga Kiswahili akieleza mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ambaye amezungumza na mwandaaji mwenza wa kongamano hilo Dkt. Kisembo Ronex Tendo, Mkurugenzi wa shirika la Afrika Mashariki Fest.

  1. Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.
  2. Katika Ukanda wa Gaza ambako Rolando Gomez, Mkuu wa Mawasiliano kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi, amezungumza na waandishi wa habari akimnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisema lazima kuepusha gharama zozote zinazoweza kuibuka iwapo uhasama utaanza upya Gaza kwani italeta janga kubwa.
  3. Na akihutubia viongozi huko Paris Ufaransa kwenye mkutano wa Kuchukua Hatua kwa Akili Mnemba ili inufaishe wote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza udharura kwa dunia kuwa tayari kukabiliana na changamoto zitokanazo na teknolojia hiyo iliyo mikononi mwa wachache licha ya kuleta mapinduzi kwenye sekta lukuki kama vile elimu, afya, na kilimo.
  4. Mashinani mashinani fursa ni yake Tiphaine Lucas, mwanamke Mratibu wa Mpango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kuhusu kutegua mabomu na Ukarabati wa Ardhi nchini Ukraine, akitumia sayansi na teknolojia kukagua sampuli za udongo katika ardhi ya Kiukreni ya kilimo iliyoathiriwa na mabaki ya vita na silaha zilizolipuka, sehemu kuu ya kazi yake hatarishi.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  

Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
10'53"