23 DESEMBA 2024
Pakua
- Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete.
- Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria.
- Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Zimbabwe kumulika nuru iliyofikia wakulima baada ya Umoja wa Mataifa kuona jinsi mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri shughuli za kilimo.
- Mashinani fursa ni yake Rukia, kijana wa kike kutoka Tana River nchini Kenya ambaye kupitia mafunzo na uwezeshaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, yeye hasiti kutoa tahadhari za mapema na kuwahamasisha jamii kujiepusha na madhara panapotokea majanga ya mabadiliko ya tabianchi.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Anold Kayanda
Sauti
10'