21 OKTOBA 2024
Pakua
- Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.
- Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.
- Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.
- Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
9'58"