Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 OKTOBA 2024

18 OKTOBA 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia eneo linalokaliwa kwa mbavu la Kipalestina, na ndoto Mchezaji kijana wa soka zilizokatizwa na vita katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Kenya, kulikoni?

  1. Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina leo imesema mataifa yote na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni amoja na Umoja wa Mataifa, wana wajibu chini ya sheria za kimataifa wa kukomesha uwepo haramu wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, wakati mashambulizi Gaza yakishika kazi na kuongeza madhila kwa raia.
  2. Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.
  3. Makala inatupeleka Tanzania hususan mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki ambako Assumpta Massoi amezungumza na mhifadhi wa mbegu za asili, mahojiano yaliyofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini humo. Mhifadhi mbegu anaanza kwa kujitambulisha.
  4. Na mashinani fursa ni yake Nosizi Reuben Dube ambaye kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), amefanikiwa kupata shahada ya chuo kikuu, akiwakilisha tumaini kwa jamii yake, ambayo imeishi Kenya kwa zaidi ya 50 bila uraia hadi walipotambuliwa hivi karibuni na serikali ya Kenya na kuwapatia vyeti vya uraia

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'38"