Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 OKTOBA 2024

09 OKTOBA 2024

Pakua

Hii leo jaridani ikiwa ni siku ya posta duniani tunaangazia huduma za posta na juhudi za mashirika za kukabiliana na Mpox nchini DRC. Makala tunasalia huko huko DRC kufuatilia uzinduzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo huo, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon.

  1. Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani.
  2. Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo.
  3. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo chanjo dhidi ya mpox imeanza.
  4. Na mashinani tutaelekea Lebabon ambapo, tutasikia simulizi ya Wahiba mwanamke mkimbizi kutoka Syria anayeishi Lebanon, ambaye      sasa amelazimika kuikimbia Lebanon kufuatia mashambulizi nchini humo.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
9'59"