02 OCTOBA 2024
Pakua
- Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa amezitaka nchi kubadilisha kuwa uhalisia ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
- Umoja wa Mataifa kila uchao unapigia chepuo wadau mbali mbali wakiwemo waandishi wa habari kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs ili sio tu yaweze kufahamika bali pia wale wanaowajibika kuyatekeleza wafanye hivyo ili hatimaye maisha ya wananchi yawe bora na si bora maisha.
- Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, iliyoanzishwa ili kuwasaidia watoto hususani vijana balehe. Je, inawasaidia vipi? Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na mwanzilishi na mkurugenzi mtendajiwa taasisi hiyo Vivian Joseph ambaye anaanza kwa kufafanua kuhusu taasisi hiyo ya Watoto Afrika Initiative.
- Katikashinani fursa ni yake Teyban Mohammed kutoka Amhara, Ethiopia, mama aliyenufaika kwa vocha za milo mbalimbali yenye lishe bora kutoka kwa WFP, akieleza manufaa ya mradi huu kwa watoto pamoja na kina mama wajawazito na wanaonyonyesha?
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'59"