Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana - Tumechoka na maneno ya viongozi sasa tunataka vitendo

Vijana - Tumechoka na maneno ya viongozi sasa tunataka vitendo

Pakua

Jana Jumapili ya Septemba 22 viongozi wa dunia walipitisha Mkataba wa Zama Zijazo. Mkataba huu unalenga kukabili changamoto za karne ya 21 kuanzia mizozo, mabadiliko ya tabianchi, haki za binadamu, hadi taarifa potofu na za uongo. Maeneo Matano makuu ni pamoja na maendeleo endelevu, amani na usalama duniani, sayansi na teknolojia, vijana na vizazi vijavyo na marekebisho ya usimamizi wa dunia, kipengele muhimu wakati huu ambapo taasisi za fedha za kimataifa na Umoja wa Mataifa wenyewe wameshindwa kuja na majawabu ya karne ya 21. Mkataba wa Kimataifa wa Kidijitali unaoelenga pamoja na mambo mengine usimamizi bora wa Akili Mnemba, pamoja na Azimio kwa ajili ya Vizazi Vijavyo linalotaka serikali za sasa kutilia maanani vizazi vijavyo zinapopitisha maamuzi yao ya leo, ni sehemu ya viambatanishi vya Mkataba huu wa Zama Zijazo. Assumpta Massoi ametaka kufahamu maoni ya vijana baada ya hatua hii, na ndio mada yetu kwa kina siku ya leo. 

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi/Anold Kayanda
Audio Duration
7'27"
Photo Credit
UN News