10 SEPTEMBA 2024
Pakua
- Miaka 63 tangu kifo cha ajali ya ndege cha Katibu Mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld huko Ndola Zambia, bado majibu hayajapatikana ya nini kilisababisha ajali hiyo wakati akielekea kusaka amani kwa iliyokuwa Congo, sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema kampeni ya chanjo eneo la kaskazini mwa Gaza imeendelea leo jumanne licha ya tukio la jana la jeshi la Israeli kuzuia kwa saa nane msafara wa wafanyakazi waliokuwa wanasafiri kwenda kutoa huduma hiyo.
- Na leo septemba 10, mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA78 unakunja jamvi baada ya mwaka mzima wa mikutano na mijadala, na hivyo kuashiria kuanza kwa mkutano wa 79 ambapo kuanzia tarehe 22 vitaanza vikao vya ngazi ya juu na Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu. Rais anayemaliza muda wake ni Balozi Dennis Francis kutoka Trinidad na Tobago na anayempatia kijiti ni Philemon Yang kutoka Cameroon.
- Katika mashinani, tunamulika mwaka mmoja tangu kimbunga Daniel kipige mji wa Dema mashariki mwa Libya na vitongoji vyake na kuleta mvua kubwa iliyosababisha mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 5,000, na kuacha makovu hadi sasa. Maelezo ya Hawa Bu Zqeeba aliyempoteza baba yake katika mafuriko hayo yanakupatia taswira halisi ya makovu.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'58"