Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 SEPTEMBA 2024

09 SEPTEMBA 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia suala la elimu katika maeneo ya migogoro, na msaada wa kibinadamu huko Upper Nile nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni??

  1. Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii.
  2. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
  3. Makala inatupeleka Maiduguri nchini Nigeria kusikia namna mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wanarejesha matumaini kwa waliokosa elimu rasmi hasa kutokana na hali mbayá ya usalama katika maeneo yao.
  4. Na katika mashinani, fursa ni yake Faeza, mfanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza biskuti nchini Afghanistan, mradi unaowezeshwa na shirika la WFP akitueleza manufaa ya mradi huo kwa jamii iliyoathirika na vita hasa wanawake na watoto.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
9'58"