Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 AGOSTI 2024

05 AGOSTI 2024

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameonya juu ya ongezeko la hatari ya kusambaa kwa mzozo Mashariki ya Kati na kuzitaka pande zote husika kutoa kipaumbele cha kuwalinda raia

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania limetumia ukurasa wake wa X,  kuelezea mambo muhimu matatu ya manufaa ya maziwa ya mama kwa mtoto. 

-Makala yetu leo inatupeleka Gaza ambako shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema wagonjwa 85 kutoka Gaza wamesafirishwa kwenda kupata matibabu huko Abu Dhabi katika Falme za kiarabu.

-Na mashinani mwanaharakati Plamedie Ndaya kutoka Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anawashauri wanawake wa Afrika kupigania kutambuliwa kwa haki zao.

Audio Duration
9'53"