Watu 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi Al- Fasher Sudan, UN yalaani vikali
Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidi
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Asante Leah katika taarifa hiyo aliyoitoa mjini Port Sudan Nkweta- Salami amelaani vikali muaji hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki. Amesema "Nimehuzunishwa sana na mashambulizi haya ya kutisha dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia kama vile hospitali, nyumba na masoko. Miundombinu ya kiraia haipaswi kamwe kulengwa na inalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu. Umoja wa Mataifa nchini Sudan unalaani vikali mashambulizi haya ya kiholela na tunatuma rambirambi zetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.”
Ameongeza kuwa mashambulizi hayo ya Al Fasher yamewashtukiza watu kwani mji ulikuwa umetulia kwa karibu wimbi mbili hali iliyoruhusu masoko kufunguliwa na familia nyingi kuendelea na maisha.
Kurejea kwa hali ya kuweza kutafuta riziki kwa watu na shughuli nyingine za kiuchumi, ufikishaji wa msaada wa kibinadamu usiozuiliwa na ongezeko la ufadhili wa kibinadamu ni muhimu kwa Sudan ili kuepusha tishio linalokuja la njaa. Amesema Nkweta- Salami.
Ameendelea kusema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na viwango vibaya zaidi vya uhaba wa chakula katika historia yake, huku zaidi ya nusu ya wakazi wake sawa na watu milioni 25.6 wakiwa na njaa kali, wengine milioni 8.5 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya njaa na wakati zaidi ya watu 755,000 wako katika hali ya janga katika majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Kaskazini, Blue Nile, Al Jazirah, na Khartoum.
Tangu kuzuka kwa mzozo mpya Aprili mwaka jana zaidi ya watu 18,800 wameuawa, zaidi ya 33,000 kujeruhiwa na watu zaidi ya milioni 10 wamezikimbia nyumba zao na miongini mwao zaidi milioni 5 wakivuka mpka na Kwenda kusaka usalama nchi za jirani.
Nkweta-Salami ametoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kukomesha mapigano mara moja na kuwalinda raia kwa gharama yoyote.
Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidi
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Asante Leah katika taarifa hiyo aliyoitoa mjini Port Sudan Nkweta- Salami amelaani vikali muaji hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki . Amesema "Nimehuzunishwa sana na mashambulizi haya ya kutisha dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia kama vile hospitali, nyumba na masoko. Miundombinu ya kiraia haipaswi kamwe kulengwa na inalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu. Umoja wa Mataifa nchini Sudan unalaani vikali mashambulizi haya ya kiholela na tunatuma rambirambi zetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.”