Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 JANUARI 2024

08 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia vita katika ukanda wa Gaza, na huduma za afya na umaskini nchini Nigeria. Makala na mashinani tunamulika ukulima bunifu na wa umwagiliaji unaosaidia wakulima wadogo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Kenya.

  1. Ikiwa leo ni siku ya 93 tangu mapigano yaanze huko Ukanda wa Gaza kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina waliojihami, likiwemo kundi la Hamas, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanazungumzia uwepo wa idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wanawake na watoto huku yakisihi timu za madaktari ziruhusiwe kuingia eneo la Gaza ili ziendelee na jukumu la kuokoa maisha. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuandalia ripoti hii.
  2. Nchini Nigeria katika Jimbo la Anambra shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika kwakushirikiana na mpango wa Bima ya Afya ya Serikali wanabadilisha maisha ya wananchi kwa kulipia sehemu kubwa ya gharama za matibabu ili kuhakikisha kila mtu anaweza kupata huduma za afya bila kudumbukia katika umaskini.
  3. Makala leo tunabisha hodi eneo la Murang’a katika kaunti ya Kiambu, nchini Kenya ambapo tunakutana na Francis Njoroge, mkulima mdogo mmoja wa mamilioni ya wakulima wadogo walioathiriwa na mabadiliko ya tabianchi lakini kupitia ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya kilimo, IFAD, anasimulia jinsi ukulima wake umeimarika. 
  4. Na mashinani tunasalia nchini Kenya mada huo wa ukulima na tunakwenda Kibera, kusikia ujumbe kuhusu mbinu bunifu ya kilimo inayoleta tija kwa wakaazi.   

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'50"